Namna Madeni Yana Umiza Na Namna Ya Kuyashinda
Hatua 10 za Kuondoka Kwenye Madeni 1. Kubali na Kiri Madeni Yote Andika kila deni ulilonalo, kiasi, riba na tarehe za malipo. 2. Tengeneza Bajeti ya Mwezi Pangilia mapato na matumizi yako kwa uwazi kabisa. Hakikisha mapato yanazidi matumizi. 3. Kipaumbele: Malipo ya Madeni Amua ni deni lipi ulipe kwanza: la riba kubwa au la kiasi kidogo. 4. Lipa Zaidi ya Kiwango cha Chini Usilipa tu kiwango cha chini, ongeza kiasi kidogo zaidi kadri ya uwezo wako. 5. Punguza Matumizi Yasiyo ya Lazima Katakata anasa, vitu vya kifahari, na matumizi yasiyo ya lazima. 6. Tafuta Chanzo Kingine cha Kipato Fanya kazi za ziada, biashara ndogo, au tumia vipaji vyako kuongeza pesa. 7. Acha Kuchukua Madeni Mapya Hakikisha huazimi tena pesa yoyote hadi umalize yote uliyonayo. 8. Weka Akiba Kidogo Kidogo Hata kama ni kidogo sana kwa mwezi, weka akiba ili kuepuka kurudia madeni kwa dharura ndogo. 9. Fuatilia Maendeleo Yako Kila Wiki Kagua maendeleo yako kila mwisho wa wiki: je, umepunguza kiasi gani? 10. Jiwek...