SALA YA TOBA BAADA YA DHAMBI YA UZINZI

SALA YA TOBA BAADA YA DHAMBI YA UZINZI


Ee Baba wa mbinguni,

Naja mbele zako sasa nikiwa na moyo uliovunjika, nikiwa na maumivu moyoni kwa sababu nimekosa mbele zako. Nimeanguka katika dhambi ya uzinzi, nami najua kuwa nimekuhuzunisha, Mungu wangu mtakatifu.

Ninakiri dhambi yangu mbele zako bila kuficha kitu. Umenipa mwili wangu kama hekalu la Roho Mtakatifu, lakini nimetumia vibaya neema yako. Ee Bwana, usiniache.

Naomba unisamehe. Nioshe kwa damu ya Yesu Kristo, mwanao, aliyekufa kwa ajili ya dhambi zangu msalabani. Ninatubu kwa moyo wangu wote, naahidi kuachana kabisa na dhambi hii.

Nirudishe tena katika hali ya usafi, unipe moyo mpya, unifanye kiumbe kipya. Naomba nguvu ya Roho Mtakatifu ili nisirudie tena dhambi hii, bali niishi maisha ya utakatifu yanayokupendeza.


Neno lako linasema:

> "Kama tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote."

— 1 Yohana 1:9


Na tena linasema:

> "Basi tubuni mkageuke, ili dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati za kuburudika kutoka kwa Bwana."

— Matendo ya Mitume 3:19


Asante Baba kwa msamaha wako. Ninalipokea kwa imani, na kuanzia sasa natembea katika upya wa maisha.

Katika jina la Yesu Kristo,

Amina.


Comments

Popular posts from this blog

MAOMBI 10 YA USHINDI

HOW TO ATTRACT THE ANOINTING

Namna Madeni Yana Umiza Na Namna Ya Kuyashinda